Female rapa Nicki Minaj amefunguka kuhusu uhusiano wake na rapa Meek Mill kwamba Mama yake hakukubali awe na uhusiano wa kimapenzi na rapa huyo.
“Kwa mara ya kwanza Mama aliposikia natoka na Meek Mill alishtuka na kusema Meek Mill hafai kuwa na mimi kwani ni rapa muhuni asiye na maadili ” alisema Nicki Minaj.
Meek Mill hakuonekana muhuni sio tu kwa Mama mkwe wake bali pia kwa Pasto wa Kanisa analosalia Nicki Minaj.
Nicki alisema stori za Meek Mill kwenda jela na habari zilizosambaa mitaani kuhusu utukutu wa rapa huyo zilizidi kumkatisha tamaa Mama yake.
Lakini kwa sasa Meek Mill ameonyesha wazi kwamba ni kijana mwema na Mama yake Nick amemkubali rasmi huku akitoa Baraka zake uwepo wa ndoa baina ya rapa huyo kutoka Philadelphia nchini Marekani.
Nicki pia aliweka wazi kwamba alikuwa na feeling na rapa huyo hata kabla hajaenda jela, na kipindi yupo jela alijisikia vibaya sana na kumuombea atoke haraka.
“Nilimpenda sana Meek Mill na nilipoongea naye kwa mara ya kwanza kwa njia ya simu alipokuwa jela nafikiri ndipo pale mapenzi yetu yalipoanza rasmi, ndio maana alipotoka haikuchukua muda mimi na yeye kujiachia pamoja” alizidi kufunguka Nicki Minaj.
Post a Comment