Sarah na Jaden


Mtoto wa Will Smith, Jaden Smith hivi karibuni ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na mrembo ambaye kwa macho anaoenekana kuwa mpole asiye na hatia usoni, lakini hali hiyo imebainika kuwa tofauti hivi karibuni.
Mrembo huyo anaeitwa Sarah Snyder mwenye umri wa miaka 19 amegundulika kuwa anahusishwa na tuhuma za wizi na analisaidia jeshi la polisi.


Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Page Six, polisi walimkamata Sarah Juni 15 mwaka huu kwa tuhuma za kuiba begi kwenye duka moja kubwa jijini New York mwezi Februari mwaka huu.



Imeelezwa kuwa mrembo huyo anaonesha ushirikiano mzuri kwa jeshi la polisi katika tangu alipokamatwa Juni 15.
Mashabiki wa Jaden wameshangazwa na tuhuma hizo dhidi ya Sarah kwa kuwa kwa mwenekano wake walimuona kuwa msichana mtulivu na asiye na hatia kwa kulinganisha na mdogo wake Kim Kardashian, Kylie Jenner ambaye hivi sasa ana uhusiano na Tyga.
Jaden Smith alitajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kylie mwaka 2013.

Post a Comment