Baraza la mazingira NEMC limekifungia kiwanda cha wachina cha Group Six kilichopo mikocheni viwandani jijini Dar es Salaam kinachojishughulisha na kazi za ujenzi ikiwemo kuchanganya zege,na kufyatua tofali pamoja na faini ya milioni 60.kutokana na kuendesha shughuli zao bila kuwa na kibali cha NEMC na Osha.
Akizungumza na Tambarare Halisi mwanasheria wa baraza la mazingira NEMC Bw.Heche suguta amesema kiwanda hicho kimekuwa kikifanya shughuli zake za uzalishaji na kuathiri afya za wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na viwanda vingine kwa kutimua vumbi pia kiwanda hicho kimekuwa kikisababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo na kuwataka  kufuata sheria za nchi na kuaacha dharau kwa maofisa wa serikali.
 
Akiongea na maafisa  hao mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho ambaye hakutaka kutaja jina lake, ameonekana kutotambua mamlaka  zinazotoa vibali nakusema wako katika majaribio na kuonesha dharau kwa maafisa hao.
 
Naye mkaguzi  wa majenzi kutoka Osha,mhandisi Swalehe Kasela amelalamikia kuwepo kwa wawekezaji wasiofata sheria za nchi,kwa mujibu ya sheria ya Osha ya mwaka 2003 inayomtaka mwekezaji kufika Osha mara tu anapokuwa na wazo la kuanzisha kiwanda.
 
Nao wafanyakazi wa kiwanda hicho ambao wameongea kwa mashrti ya kutopigwa picha kwa kulinnda ajira zao ,wamelalamikia kutokuwepo kwa vifaa vya kufanyia kazi,na msilahi madogo ambyo hayalingani na kazi ikiwa ni kulipwa ujira wa shilingi ishirini kwa kubeba tofali ambapo wanatakiwa kubeba tofali mia 500 kwa siku.
Katika hali isiyo ya kawaida,katika zoezi hilo Tambarare Halisi imegundua licha  ya kuwepo kwa uzalishaji wa Zege na Tofali biashara ya uuzaji wa vigae katika kiwanda hicho umekuwa ukifanyika,ambapo mwansheria wa NEMC ameiomba serikali kufatilia kwa karibu kama biashara hiyo inalipiwa kodi.
 
Katika  hatua nyingine ITV imebaini eneo maalum ambalo wekezaji hao wameweka ngazi ya kupitia wanapowakimbia maafisa wa serikali.
 
Malori yanayoleta vifaa katika kiwanda hicho cha G SIX  kimesababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wengene wa barabara kwa kukosa pa kupita katika eneo hilo kutokana na mojawapo ya lori lililoleta kokoto kiwandani hapo kuharibika katikati ya barabara huku juhudi za ziada za kutoa lori hilo zikiwa zinasua sua.
 

Post a Comment