Mgombea ubunge kupitia chama
cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) jimbo la kahma mjini James Lembel katika mikutano yake ya
kampeni iliofanyika katika kata za Mwendakulima na Nyasubi wilayani humo.
Lembeli amesema kiongozi
bora ni Yule anayetekeleza maendeleo na sio kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki.
Amesema endapo wananchi
watachagua chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, watahakikisha serikali
hiyo inatatua matatizo ya wananchi kwa kuwekeza katika elimu na upatikanaji wa
huduma za afya.
Amesema elimu ndio urithi
pekee kwa mtoto, hivyo Chadema imejipanga kuhakikisha inatoa elimu bure ili
kuwasaidia watanzania kuondokana na umasikini unaochangiwa na kukosa elimu.
Akiwa katika kijiji cha Busalala
kata ya Mwendakulima, Lembeli amewapongeza wananchi kwa kushirikiana nae katika
uongozi wake uliopita, katika ujenzi wa shule ya msingi Busalala iliyopo katani
humo.
Kwa upande wake mwenyekiti
wa CHADEMA wilayani humo Juma Protas amewataka wananchi kupuuza wanasiasa
wanaowapotosha wananchi kwa kuwapa pesa na vitu vidogovidogo ili wasiende
kupiga kura.
Protas amesema vitendo hivyo
ni ukiukwaji wa haki za msingi na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano mara
wanasiasa hao wanapojitokeza ili kuwabaini na kuchukuliwa hatua.
Post a Comment