Njia 9 Za Kutengeneza Lips Laini Zenye Mvuto.

Njia 9 Za Kutengeneza Lips Laini Zenye Mvuto

Watu wengi hasa wanawake wanapenda kuwa na midomo laini yenye mvuto wa kimahaba. Lakini kutokana na asili ya mtu na hali ya hewa, vimepelekea wengine kuwa na midomo migumu isiyovutia hasa katika swala zima la mahaba.
Hata hivyo kama wewe ni mwathirika wa tatizo hili na kwa maana nyingine hata imekupelekea  kuzikatia tamaa lips zako, leo nina njia za asili na kisasa za kuzitengeneza lips zako katika muonekana na mvuto unaopendelea. Bila kupoteza muda tuanze kwa kuzitazama Njia 9 Za Kutengeneza Lips Laini Zenye Mvuto.

Njia 9 Za Kutengeneza Lips Laini Zenye Mvuto.

1. Kunywa maji mengi.
Ukosefu wa maji mwilini si mzuri kwa afya ya ngozi yako. Njia nzuri ya kukuza afya ya ngozi yako ni kwa kunywa maji mengi kila siku. Hii itakusaidia kuboresha ngozi yako, kukuza seli mpya na kuweka ngozi yako hali ya unyevu.

2. Sugua lips zako kwa kutumia vipande vya Tango.

Kusugua midomo yako kwa kutumia vipande vya tango, itasaidia kulainisha na kuzing’alisha lips zako. Matango yana  vikemikali asilia aina ya phytochemicals ambayo itasaidia kulainisha na kunyevua midomo yako.

3.  Tumia mafuta ya Nazi.

Mafuta ya nazi yana matokeo mazuri sana katika ngozi ya mwanadamu. Paka kiasi kidogo tu cha mafuta ya nazi kwenye midomo yako itasaidia kulainisha na kuiweka midomo yako katika hali ya kuvutia.

4. Paka mafuta ya petroleum jelly kabla ya kwenda kulala.

Kupaka mafuta ya petroli jelly muda mfupi kabla ya kwenda kulala itasaidia kunyevua midomo yako. Ukijiwekea mazoea ya kufanya hivi kwa muda mrefu, itakusaidia kuongeza ulaini wa midomo yako na kuifanya kuwa na muonekano wa kuvutia sana.

5. Tumia lipstick ya kunyevua lips zako.

Lipstick za kunyevua midomo zinasaidia kulainisha midomo yako, lipstick hizo zimetengenezwa kwa siagi ya kakao, siagi ya shea na mafuta ya nazi amabyo husaidia kulainisha midomo yako.

6. Tumia Lip Balms Zinazosaidia Kukulinda kutokana na athali za mionzi ya jua.

Jua kali ni adui wa ngozi yako, na hapa najumuisha ngozi ya midomo yako pia. Ili kuzuia athari za mionzi ya jua kwenye lips zako nakushauri kutumia bidhaa zenye SPF 15 (Sun Protection Factor).

7. Tumia mchanganyo wa asali na sukari.

Tengeneza mchanganyo wa asali na sukari, kisha paka kwenye lips zako kwa dakika kadhaa. Hii itasaidia kuiweka ngozi ya midomo yako nyororo na laini, pia husaidia kuondoa seli za ngozi zilizokufa.

8. Tumia vyakula vya kujeng mwili.

Ili upate lips laini na za kuvutia ni muhimu sana kupata vyakula vya kujenga mwili, vyakula kama samaki, mayai, nyama, mboga za majani na matunda ni muhimu sana kwa afya ya ngozi yako kwani vina vitamini B na C ambazo ni muhimu sana kwa Afya ya ngozi yako. Pia samaki ni muhimu sana kwani ina omega-3 fatty acids ambayo ni muhimu kwaajili ya kusawazisha ngozi yako.

9. Acha tabia ya kuuma lips zako na kung’ata kucha kama unapenda kuiweka midomo yako laini na yenye mvuto.

Ni muhimu sana kutengeneza midomo yako katika hali ya ulaini na mvuto kwani ni muhimu sana na huleta utamu wa pekee hasa katika suala zima la mahaba. Ninayo imani kuwa  njia zilizotajwa hapo juu zitakusaidia kuzitengeneza lips zako laini na zenye mvuto wa kimahaba.
Je Unayo nyongeza yoyote kuhusu njia hizi tuandikie katika box letu la maoni hapo chini!!

Post a Comment