September 29 michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya
iliendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti,
miongoni mwa mechi zilizovuta hisia za watu wengi ni mechi ya Arsenal dhidi ya Olympiakos, mechi ambayo ilimalizika kwa klabu ya Arsenal kupoteza mechi hiyo katika uwanja wake wa nyumbani kwa jumla ya goli 2-3.
Mchezo mwingine uliokuwa ukivutia ni mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Bayer Leverkusen mechi ambayo ilimalizika kwa klabu ya FC Barcelona kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-1 mechi iliyochezwa katika uwanja wa Camp Nou.
FC Bayern Munich walikuwa wenyeji wa Dinamo Zagreb katika uwanja wa Allianz Arena, mchezo ambao ulimalizika kwa FC Bayern Munich kuibuka na ushindi wa idadi kubwa ya magoli kwani ilishinda jumla ya goli 5-0.
Klabu ya Chelsea chini ya kocha wake Jose Mourinho walisafiri hadi Ureno kuifuata FC Porto katika uwanja wa Estadio do Dragao, mahali ambapo Jose Mourinho ana historia na heshima kubwa katika uwanja huo ila kwa bahati mbaya Chelsea walipoteza mchezo huo kwa jumla ya goli 2-1.
Post a Comment