Kitendo cha mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kutupia mtandaoni video inayomuonesha mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ au Mama Tiffah akioga bafuni, kimetafsiriwa kuwa ni kumuabisha mzazi mwenziye huyo.
NI NDANI YA WHITE HOUSE
Video hiyo ya hivi karibuni, inadaiwa Diamond aliitupia kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram kisha kuitoa muda mfupi bila kujua imeshachukuliwa na wajanja.
Katika video hiyo, Zari anaonekana akiwa kwenye lile bafu lao jeupe, lililonakshiwa kwa dhahabu ndani ya mjengo wao (white house) uliopo Madale jijini Dar.
ZARI AOGA AKITAZAMA RUNINGA
Video hiyo ya sekunde kadhaa ambayo gazeti hili linashikilia nakala yake, iliyoibua tafrani kubwa ikiwa ni siku chache tangu Zari amzalie Diamond mtoto wa kike, Latifah Nasibu ‘Princess Tiffah’.
Video hiyo ilimuonesha Zari akioga kwa raha zake, huku akitazama runinga kubwa iliyopo bafuni humo.
NI KINYUME NA MAADILI
Mara baada ya kusambaa kwa video hiyo ndipo kukaibuka gumzo mitandaoni huku wengine wakisema kuwa hakupaswa kuweka video hiyo na kwamba amemwanika Zari kinyume na maadili ya Kibongo.
WAKWE WAIONA
Habari kutoka kwa chanzo ambacho ni mtu wa ndani kwa Diamond zilieleza kwamba, jamaa huyo aliitoa video hiyo baada ya wakwe na ndugu wa Zari kuiona na kwamba hawakupendezwa nayo.
“Si uliona ameitoa fasta, Zari alimwambia kuwa atoe maana upande wake hawakufurahishwa,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa gazetini.
MAONI YA ‘WAPENDA UBUYU’
Kufuatia ishu hiyo, ‘wapenda ubuyu’ walimvaa Diamond ambapo kila mmoja alikuwa na maoni yake juu ya video hiyo.
“Nooo… hakupaswa kumwanika. Kwanza ni ili iweje?
“Kweli ni kumuabisha mama Tiffah au anataka kumfanyia kama Wema (Sepetu) kipindi kile alimrekodi akimbembeleza usiku kisha akaisambaza sauti?
“Sasa nashindwa kuelewa, hivi sasa ndiyo anamwanika hivyo wakati ni mke wake?
“Waacheni watu na maisha yao, mbona Kim (Kardashian) na Kanye wanatupia tu kila siku na maisha yanaendelea? Acheni ushamba bwana.
“Mambo mengine bora wakaacha uzungu,” ilisomeka sehemu ya maoni hayo mengi.
DIAMOND ANASEMAJE?
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, gazeti hili lilimsaka Diamond kwa njia mbalimbali ikiwemo kumtafuta kwa njia ya WhatsAPP na kumuuliza ishu hiyo lakini hakujibu.
NI AIBU NYINGINE KWA ZARI
Ukiacha tukio la Februari mwaka huu, ambapo Zari alitupia tena akiwa anaoga bafuni, miezi kadhaa alidaiwa kurekodiwa mkanda wa utupu ambao ulidaiwa kusambazwa mitandaoni na aliyekuwa mumewe, Ivan Ssemwanga na swahiba wake, King Lawrence ikiwa ni mwendelezo wa kumchafua.
Kwa upande wake Zari amekuwa mtu wa kukaa kimya kwa maana ni mtu wa kupotezea (never mind).
Post a Comment