Mgombea
urais kupitia chama cha mapinduzi CCM Dr John Pombe Magufuli amewaambia
watanzania kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuwatumikia
watanzania na kuwataka watendaji wanaotoa taarifa za uongo kwa viongozi
waandamizi kuacha tabia hiyo kwa kuwa anazifahamu vyema changamoto na
shida za watanzania.
Dr Magufuli ameyasema hayo katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera
wakati akihitimisha ziara ya kampeni ya kusaka ridhaa ya watanzania kuwa
rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuongeza kuwa ameamua
kutumia usafiri wa barabara ili kujionea na kuzifahamu changamoto za
wananchi hasa wa hali ya chini ili aweze kuzitatua na kuwatahadharisha
watendaji wanaotoa taarifa za uongo lakini pia akaongeza kuwa serikali
yake endapo itapata ridhaa ya watanzania imejipanga kuligeuza eneo la
Ngara kuwa eneo la kimkakati kibiashara kutokana na jiografia yake na
uwepo wa madini aina ya nikel.
Aidha Dr Magufuli ameendelea kusisitiza kutumia vyema na kwa
uadilifu rasilimali za nchi ili kufufua na kujenga viwanda
vitakavyosaidia kupunguza tatizo la ajira hususani kwa vijana na kuwa na
nchi inayotegemea uchumi wa viwanda.
Dr Magufuli amehitimisha ziara za kampeni katika mkoa wa Kagera
ambapo amefanya mikutano katika maeneo ya Misenyi, Kayanga, Kyerwa na
hatimae Ngara achilia mbali mikutano ya barabarani alikokuwa
akisimamishwa na wananchi huku kiongozi wa msafara alhaji Bulembo
akizungumzia kero ya uwepo wa vizuizi vingi barabarani.
Post a Comment