Mamlaka
ya chakula na dawa TFDA kanda ya nyanda za juu kusini, imeteketeza
vyakula na vinywaji vilivyopitwa na muda wa matumizi pamoja na vipodozi
ambavyo vimepigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu kwa vile vina
kemikali zenye sumu,vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni
kumi,vilivyokamatwa kwenye maduka mbalimbali katika manispaa ya
sumbawanga mkoani Rukwa.
Mkaguzi wa Dawa wa mamlaka ya chakula na Dawa TFDA kanda ya nyanda
za juu kusini Dakta Sylvester Mwidunda, akiongea wakati wa uteketezaji
wa bidhaa hizo zenye madhara makubwa kwa matumizi ya binadamu,amesema
msako huo ni endelevu kwa vile baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa sio
waaminifu,na kwamba wamegundua kiwanda kidogo kinachotengeneza pipi bila
ya kufuata taratibu na sheria, na kuweka anuani ya moshi kwa
udanganyifu.
Naye afisa afya na usafi wa mazingira wa manispaa ya Sumbawanga
Bw.sward Temba, amesema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa
wakikamatwa zaidi ya mara moja wakitenda kosa la kuuza vyakula ambavyo
vimepitwa na tarehe zake za matumizi na pia vipodozi ambavyo vina sumu
na vimepigwa marufuku,na kwamba sasa badala ya kuchangia gharama za
uteketezaji wa bidhaa hizo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa
ni pamoja na kufikishwa vyombo vya kisheria.
Post a Comment