Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, January Makamba amewaasa watanzania kutovunja umoja na amani ya taifa kwa sababu ya uchaguzi mkuu huku akilitumia neno ‘lofa’ kwa njia chanya.

Makamba ametumia akaunti yake ya Twitter kuwakumbusha watanzania kuwa maisha yanaendelea baada ya uchaguzi mkuu hivyo hakuna haja ya kutengeneza nyufa kwa na kupoteza umoja tulionao.

Hichi ndicho alichoandika Twitter
Uchaguzi ukisha Kuna taifa Ugomvi ukisha Kuna maisha Kuweka nyufa Si sifa Taifa likifa Nani si lofa? Bila taifa Mshindi ni lofa

Post a Comment