Mshambuliaji wa kitanzania anayesukuma soka la kulipwa jamuhuri
ya Kidemokrasia Kongo kwenye klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta,
amesema Taifa Stars haijapoteza dira ya kucheza fainali za mataifa ya
barani Afrika za mwaka 2017 zitakazochezwa nchini Gabon.
Samatta, amesisitia suala hilo alipokua akizungumzia mchezo wa kesho
ambapo Taifa Stars watakua nyumbani kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es
salaam wakipambana na timu ya taifa ya Nigeria katika mchezo wa kuwania
kufuzu fainali za Afrika.
Amesema kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Misri haikumaanisha kama
Taifa Stara ilipoteza dira ya kufanya vizuri kwenye michezo itakayofuata
ya kundi la saba, na badala yake anaamini ni wakati mzuri kwa wachezaji
wenzake pamoja na mashabiki wa soka nchini kuamini hivyo.
Mshambuliaji huyo ambaye huonekana kuwa tegemeo la Stars wakati wote,
amewazungumzia Nigeria ambao watakwenda kupambana nao kesho, kwa kusema
kwamba ni timu ya kawaida na hadhani kama kuna jambo linalogopesha
kuelekea katika matanange huo.
“Wao wanakuja kama wakubwa, huenda wakadharau wakijua wanapambana na
Tanzania. Lakini nakuhakikishia tutapambana na kuhakikisha tunafanya
vizuri.
“Hii ndiyo nafasi yetu, lakini Watanzania ni tegemeo letu kubwa na
wamekuwa wakitupa nguvu kila wanapojitokeza na kutuunga mkono kwa nguvu.
“Ninawaomba wajitokeze kwa nguvu kutuunga mkono na sisi tutapambana na nguvu kubwa,” alisema Samatta.
Samatta, Thomas Ulimwengu pamoja na Mrisho Ngassa wanacheza soka nje
ya nchi na tayari wameshajiunga na wachezaji wenzao kwenye kikosi cha
timu ya taifa ya Tanzania ambacho kilikua kimeweka kambi ya juma moja
nchini Uturuki.
Post a Comment