Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Chalse Boniface Mkwasa amezungumza na waandishi wa habari hii leo juu ya maandalizi ya mwisho ya Mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Nigeria utakaopigwa kesho uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


Mkwasa amesema Safu ya ushambuliaji iko vizuri na amewaombe wachezaji kukumbuka yale ambayo wamewafundisha mazoezi.’Kama watakuwa na utulivu wa kukumbuka tuliyo wafundisha nadhani tutafanya vizuri.majeruhi ni madogo Sana na ya kawaida yaliyotokea Leo hasubui Kama mchezaji Mbwana Samata’

Pia mkwasa amemshukuru rais kikwete kwa kuwa pamoja na wao,na amemuomba pia atumie fursa hii kuja uwanjani pia kuwaaga watanzania.Mkwasa pia amesema ‘Nimewaagiza wachezaji kutumia nafasi zote zitakazopatikana,ushindi ni ushindi tunahitaji magoli yeyote yatakayopatikana’.

Post a Comment