Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF – Prof. Ibrahimu
Lipumba amekana tuhuma anazodaiwa kutumika na chama tawala cha CCM
kuuvuruga umoja wa wapinzani nchini.
Wakati akihojiwa na Azam Tv kwenye taarifa ya habari hapo jana jioni,
Mwandishi alimtaka Lipumba ajibu tuhuma hizo za kutumika na chama cha
Mapinduzi CCM ili kuharibu nguvu kubwa iliyopo sasa kwa vyama vya
upinzani vinavyounda Katiba ya Wananchi – UKAWA.
“Sisi ndio wapinzani wakweli, mimi nilijiunga na CUF mwaka 1999, na
tangu hapo ndio nilikuwa mpinzani mkuu wa CCM, iweje sasa nitumike na
CCM kuua Upinzani?, situmiki na CCM “, alijibu Lipumba.
Lipumba pia amekana taarifa zilizozagaa siku ya jana kuwa alikuwa
anataka kuongea na waandishi wa habari, na kusema kwamba habari hizo
zilikuwa ni uzushi mtupu.
Source – Azam TV
Post a Comment