Aliyekuwa
rais wa Guatemala Perez Molina ambaye alijiuzulu jana ameonja machungu
ya mahabusu baada ya kulala humo usiku wa kuamkia leo kabla ya
kupandishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.
Molina amelala mahabusu ikiwa ni utekelezaji wa amri ya mmoja kati
ya majaji wa katika mahakama ya nchi hiyo ambaye aliamrisha akamatwe na
kuwekwa chini ya ulinzi wa vyombo vinavyosimamia wahalifu nchini humo
huku taratibu za kumfikisha mahakamani kukabilina na mashtaka ya
ubadhirifu zikamilishwa.
Majira ya asubuhi Molina alifikishwa mahakamani huku akizongwa na
camera za waandishi wa habari na kisha kupanda kizimbani kukabiliana na
mashtaka ambayo yanamkabili ya kulisababisha hasara taifa hilo na
kupokea rushwa vitu ambavyo ni kinyume na katiba ya Guetemala.
Katika mashataka hayo mahakamani hapo Perez Molina alidaiwa kupokea
rushwa ya dola za marekani milioni tatu nukta saba kutoka kwa
wafanyabiashara nchini humo ili aweze kutoa maagizo kwa serikali yake,
maagizo ambayo yatawasaidia wafanyabiashara hao.
Molina amefikishwa mahakamani baada ya maandamano ya muda mrefu ya
kumpinga kutokana na kudaiwa kupokea rushwa huko ambapo baada ya
maandamano hayo bunge la nchi hiyo lilimuondolea kinga ya kutoshtakiwa
na saa chache baadaye yeye kujiuzulu na kisha kukamatwa na kushtakiwa.
Post a Comment