MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imesema Waziri wa Habari, Dk. Fennela Mkangara hakufuata utaratibu wa kisheria katika kulifungia gazeti la MwanaHALISI Julai 30 miaka mitatu iliyopita.
Jaji
Salvatory Bongole amesema Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 aliyoitumia
kufungia gazeti hilo lililokuwa linachapishwa kila Jumatano na kampuni
ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), inaelekeza kuwa pamoja na hatua
nyingine kutaka maelezo ya utetezi kwa mchapishaji.
Katika
uamuzi wa shauri lililofunguliwa mara baada ya MwanaHALISI kufungiwa,
Jaji Bongole amesema gazeti hilo liko huru kuchapishwa kuanzia sasa.
Jaji
huyo amesema pamoja na uamuzi huo, kampuni iliyolalamika imepewa mafao
yote iliyoyaomba katika kufungua shauri hilo la mapitio ya uamuzi wa
Waziri – prerogative orders.
Miongoni
mwa maombi ya faida ni HHPL kulipwa gharama za kesi pamoja na fidia
kutokana na hasara iliyopatikana kwa muda wote wa gazti hilo kuwa
kifungoni.
Wakati Waziri alipofungia gazeti la MwanaHALISI, alieleza kwamba sababu ni kuandika habari na makala za uchochezi.
Habari
hasa iliyoikera serikali hata kujilazimisha kuchukua hatua hiyo katili,
ilikuwa ni iliyohusu uchunguzi wa tukio la kutekwa na kuteswa hadi
karibu na kifo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania
(TMA), Dk. Steven Ulimboka.
Dk.
Ulimboka alikumbwa na mkasa huo mnamo Juni 2012 alipotekwa usiku eneo
la Tazara, karibu na viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambako aliitwa
na mtu aliyemtaja kuwa ni ofisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye alikuwa
na mawasiliano ya karibu naye kwa saa kadhaa siku chache na usiku huo
siku ya tukio.
Daktari
huyo aliyekuwa mtumishi wa taasisi ya Marekani nchini, alifika eneo la
Tazara akifuatana na daktari mwenzake aitwaye Deo, ambaye mara baada ya
tukio hilo, wakati wa alfajiri, alimpigia simu Mhariri wa MwanaHALISI,
Jabir Idrissa, kumjulisha kuhusu kutekwa kwa Dk. Ulimboka.
Kufuatia
habari za kuachiwa huru kwa MwanaHALISI, Mhariri huyo amesema
amefurahishwa na uamuzi wa mahakama ya Tanzania, kwa kuwa umethibitisha
kosa la serikali la kujichukulia maamuzi mkononi chini ya kuvunja sheria
ilizoahidi kuzilinda.
“NImefurahi
sana kuthibitishiwa kwamba serikali ilikosea katika kufungia gazeti.
Uamuzi wa jaji umesema waziri hakufuata hatua za kisheria alizopaswa
kuchukua kabla ya kufungia gazeti, ikiwemo ya kuwapa wamiliki na mhariri
nafasi ya kujitetea,” amsema Idrissa.
“Lakini
pia uamuzi huu unatakiwa uwe funzo muhimu kwa utawala kwamba hauwezi
kudumu na kudumu kwa msisitizo wa kuhifadhi na kufurahia sheria
zilizopitwa na wakati ambazo miaka kadhaa nyuma zilishatangazwa kuwa ni
sheria kandamizi,” alisema.
Mhariri
amesema anawasiliana na mmiliki na mchapishaji wa MwanaHALISI, kampuni
ya HHPL, kukamilisha taratibu za kuchapisha toleo la kwanza haraka
iwezekanavyo. Gazeti hilo lilikuwa likichapishwa mara moja kwa wiki siku
ya Jumatano.
Post a Comment