Stori ninayotaka kukusogezea ni kutokea
kwenye siasa ambayo inamuhusu msanii wa kike wa filamu, Chuchu Hans
ambaye hivi karibuni alikuwa ni miongoni mwa wasanii wanaomsupport
mgombea wa Urais kupitia UKAWA, Edward Lowassa lakini kwa sasa msanii
huyo ameamua kukikimbia chama hicho na kuki support chama cha Mapinduzi.
Ripota wa millardayo.com alikutana na
mwenyekiti wa Mama ongea na Mwana, Steve Nyerere na kuzungumza naye
kuhusiana na msanii huyo kuhamia CCM…’Chuchu
hans alitoroka na sasa hivi amerudi nyumbani sifa ya kwanza unapotimiza
miaka 18 unaruhusiwa kwenda kujitegemea lakini ukiona maisha ni magumu
baba ni baba na mama ni Mama kwa hiyo sio dhambi mtoto kurudi nyumbani
na mimi kama Baba na Mama Samia tumempokea Chuchu Hans katika chama cha
Mapinduzi’ – Steve Nyerere
‘Chuchu Hans mpaka sasa hivi ana siku
ya tano tangu tumempokea na mganga siku zote haruhusiwi kusema kwamba
nani alikuja na mimi kama Mwenyekiti wa Mama ongea na Mwao Tanzania
siruhusiwi kusema wangapi wanahitaji kuja katika chama cha Mapinduzi
lakini viashiria vinaonesha wangapi wanahitaji kurudi’– Steve Nyerere‘Kwa hiyo Chuchu Hans kafungua milango kama Mwanamke jasiri kurudi kwa Mama yao na kaamua kurudi kwa Dkt John Pombe Magufuli sasa si dhambi hata kwa hao wengi wakiamua kurudi nyumbani huku hakuna yale maandamano, kwa hiyo ninachotaka kusema ukitaka kuishi kwa Amani cha kwanza kabisa ni lazima ujitambue na ndio maana Chuchu Hans kajitambua’ – Steve Nyerere
‘Lakini mimi nataka niwaambia wasanii wenzangu tusipotoke na hayo yansyokuja ni mchanganuo baada ya wenzetu wakiapishwa maisha mengine yanaendelea isije kutokea tukachukua tukashindwa kufanya kazi zetu huko kwenye kazi za uigizaji naomba nilisisitize hilo’ – Steve Nyerere
Post a Comment