Serikali wametakiwa kuipokea kwa mikono miwili sheria ya makosa
ya ya mtandao kwa kuwa inalenga katika kuwafaidisha zaidi kwa kuwalinda
dhidi ya wizi wa mtandaoni, udhalilishaji na kuingiliwa faragha.
Hayo yameelezwa na waziri wa Mawasiliano, Sayansi Na Teknolojia,
Profesa Makame Mbawara alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana
jijini Dar es Salaam.
Profesa Mbawara alitoa mfano wa watu wanatumia simu na mitandao
kufanya utapeli unaowapa hasara kubwa wananchi, na pia picha zisizofaa
zinazoumiza hisia za watu wanaoguswa moja kwa moja na tukio hilo.
“Picha ambazo saa nyingine kumetokea accident pahala, watu wameumia
vibaya lakini watu wanazipeleka kwenye mitandao,” alisema. “Leo tu mtu
anaamka anatuma ujumbe kila mahala, picha za matukio ya kutisha
yanayosababisha wananchi waweze kuchanganyikiwa,” aliongeza.
Aidha, Profesa Mbawara aliwataka wananchi kutodanganywa kuwa sheria
hiyo imetungwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Alifafanua kuwa
sio kweli kuwa anaepokea ujumbe wa kichochezi na zisizofaa ataingia
hatiani bali yule aliyetuma ndiye anayetakiwa kukutana na mkono wa
sheria. Alisema mtumiwaji wa meseji akifuta bila kusambaza hataingia
hatiani.
Ingawa kanuni za sheria hiyo bado hazijatungwa, Profesa Mbawara
alieleza kuwa serikali imejipanga vizuri katika kutekeleza sheria hiyo
inayoanza rasmi leo, Septemba 1.
“Serikali imejiridhisha baada ya kufanya maandalizi yote muhimu ikiwa
ni pamoja na kutoa elimu kwa umma na kujenga uelewa kwa watekelezaji wa
sheria hizi,” alisema.
Amewataka wananchi kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa manufaa ya kila mmoja kwa maendeleo ya taifa.
Post a Comment