Mgombea
urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh Edward Lowassa ameendelea na ziara
ya kunadi sera zilizoko kwenye ilani ya UKAWA katika mkoa wa Ruvuma na
kupata mapokezi makubwa na amesema akifanikiwa kuwa rais atayapatia
ufumbuzi matatizo sugu yanayowakera wananchi kwa muda mfupi na
kuhakikisha maisha yao yanabadilika.
Mh Lowassa aliyeambatana na viongozi wengine wa UKAWA wakiwa katika
mji wa Songea ambao walipokelewa na maelfu ya wananchi amesema viongozi
wa UKAWA wamejipanga kuwatumikia watanzania kwa vitendo na wala sio kwa
maneno na ahadi zisizotekelezeka.
Awali akiwa katika jimbo la Madaba Mh Lowassa aliwaomba wananchi kuona umuhimu wa kupokea mabadiliko.
Kwa upande wao viongozi wengine wa chama hicho waliambatana na Mh
Lowassa wameendelea kuwataka wananchi kupuuza maneno yanayosemwa na watu
wasiopenda mabadiliko ambayo asilimia kubwa yanalenga kuwakatisha
tamaa.
Baadhi ya wananchi na viongozi wakiwemo wa wilaya za mkoa wa Ruvuma
wamesema utaratibu wa ahadi zisizo na vitendo umechangia kuongeza
makali ya maisha ya wananchi hasa vijijini na kwamba njia pekee ya
kuondokana na tatizo hilo ni kukubali mabadiliko kwani sasa wamechoka.
Post a Comment