Baadhi ya wanamichezo duniani akiwemo Jose Mourinho, Frank Lampard na Cristiano Ronaldo wameingia katika kitabu cha kipya cha Guinness World Records
ambacho toleo jipya litatoka Septemba 10, Mastaa hao wamepewa heshima
ya kuwemo katika kitabu hicho kutokana na rekodi zao mbalimbali.
Jose Mourinho ndio ameingia katika headlines kubwa zaidi baada ya kupewa Tuzo za Guinness World Records mara nne, hivyo ana rekodi nne tofauti zitakazo mfanya aandikwe katika kitabu hicho.
Kocha huyo wa Chelsea
ameweka rekodi ya kuwa kocha wa klabu ya kwanza kumaliza msimu akiwa na
point 95, kocha aliyeshinda Kombe la Ligi ya Mabingwa mara nyingi akiwa
na klabu mbili tofauti (2), ndiye kocha mwenye umri mdogo aliyewahi
kucheza mechi 100 za Ligi ya Mabingwa ilikuwa kipindi ana miaka 49 na
siku 12,
Mourinho pia ana rekodi ya kutofungwa katika uwanja wa nyumbani mara 77 hii ni katika mechi za Ligi Kuu. Hata hivyo Cristiano Ronaldo ameingia katika rekodi ya kuwa mchezaji aliyeshinda hat-tricks 27 katika mechi za Laliga.
Beki wa klabu ya Manchester United
yumo pia kwa rekodi ya kuwa mchezaji aliyetokea benchi na kufunga goli
la mapema dakika ya 5 na sekunde 9 baada ya kuingia, ilikuwa dhidi ya Burnley msimu uliyopita, Smalling alijiongezea rekodi kwa kufunga goli la pili hivyo anatajwa kama mchezaji aliyetokea benchi na kufunga magoli mengi.
Hii ni rekodi nyingine katika michezo mtu wangu
Post a Comment