Mke wa kwanza wa Dk. Wilbroad Slaa, Bi. Rose Kamili amejitokeza
hadharani na kukananusha baadhi ya kauli alizozitoa mumewe huyo wa
zamani dhidi ya Chadema na mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaa, Bi. Rose
alidai kuwa wakati wanaishi na mumewe huyo hawakuwahi kushindia mihogo
kwa shida kama alivyodai Dk Slaa wakati akiishambulia Chadema.
“Siwezi kusema kwamba mihogo ni mibaya kuliwa lakini napenda kikri
kwamba katika maisha yetu niliyokaa na Dk Slaa kuwanzia mwaka 1986,
sikuwahi kushuhudia familia yetu ikila mihogo kwa sababu ya kukosa
chakula kama alivyosema kwenye hotuba yake,” alisema.
Bi. Rose alimshangaa Dk Slaa kwa kile alichokifanya dhidi ya Lowassa
katika hotuba yake kwa kuwa mgombea huyo wa urais wa Chadema ndiye
aliyemshauri kuhamia Chadema na kugombea ubunge wa Karatu baada ya jina
lake kukatwa na CCM.
Alieleza kuwa alichofanya Dk Slaa ni chuki binafsi na kwamba alisema
uongo kwa kutokana na chuki alizokuwa nazo dhidi ya watu wengine.
“Yeye anapomhukumu Lowassa, je yeye dhambi alizonazo ni kiasi gani, yeye amevunja ngapi ?,” alihoji Bi. Rose.
“Awaeleze watanzania, ni dhambi ngapi alizozifanya yeye, kwa sababu
ufisadi kama ni dhambi ni wizi, ni amri ya saba ya Mungu, basi uzinzi
pia ni amri ya saba ya Mungu kwamba amevunja na yeye ana dhambi. Kwa
hiyo usimnyooshee kidole mwenzako wakati na wewe una dhambi.
“Wewe unatelekeza watoto huwatunzi, ni dhambi. Unasema uongo, unasema
kwamba ‘serikali ya Chama Cha Mapinduzi imenizuia kufunga ndoa’, wakati
ni mimi. Hiyo ni dhambi, kwa nini uwaseme wale watu, kwanini uwaseme
mawaziri ambao hata siwajui wakati sisi ndio tulioweka pingamizi. Ni
dhambi, sasa yeye anamnyoshea kidole nani?
“Wakati wanahangaika sasa kuhusu Dk. Slaa, kwamba amekasirika kuachia
nafasi ya urais aliyokuwa anahitaji, asiseme kwamba alikuwa hahitaji
ile nafasi ya urais, alikuwa anaihitaji. Ndio maana walimpeleka
Ujerumani kujifunza..”
Post a Comment