Siku kadhaa baada ya waziri Mkuu mstaafu, Fredirick Sumaye kudai
kuwa ameamua kuondoka CCM kwa madai kuwa viongozi wa chama hicho
hawauoni umuhimu wake na kutomhusisha na baadhi ya mambo ya serikali,
rais Jakaya Kikwete ameyatolea majibu.
Katika majibu yake, Rais Kikwete ameeleza kuwa kiongozi anayetoka
madarakani hawezi kulazimisha kuombwa ushauri na kiongozi aliyeko
madarakani. Alisema Rais yeyote huwa amekamilika kutokana na timu ya
watu wake wanaomshauri kuhusu mambo mbalimbali lakini anaweza kuomba
ushauri kwa kiongozi aliyetoka madarakani pale anapoona inafaa na sio
lazima.
“Huwezi kulalamika kuwa huombwi ushauri,” alisema rais Kikwete na
kuongeza kuwa yeye anamalizi muda wake wa uongozi na kustaafu na kwamba
kama rais anayekuja ataona ni jambo muafaka kuomba ushauri atachangia
kwa kadri ya uwezo wake lakini kiongozi yeyote aliyestaafu hawezi
kulazimisha kuombwa ushauri.
Post a Comment