Mgombea
urais kupitia chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli amewaahidi
neema kwa wafanyakazi wote nchini wakiwemo walimu pamoja na wakulima kwa
kuwalipa mishahara inayoendana na kazi zao huku akiwaonya kufanya kazi
kwa kujituma kuliwezesha taifa kusonga mbele kwa kuwa serikali yake
haitwavumilia wafanyakazi wazembe.
Mgombea huyo wa kiti cha urais kupitia CCM ameyasema hayo kwa
wakazi wa namtumbo akiwa njiani kutokea Songea mkoani Rukwa kuelekea
Masasi mkoani Mtwara kupitia Tunduru, Mangaka Nanyumbu na hatimae
Masasi huku akisimamishwa njiani mara kwa mara na wananchi waliotaka
kumueleza kero zao ambapo pia amekagua ujenzi wa barabara unaoendelea na
kuongeza kuwa serikali yake itaboresha mishahara ya wafanyakazi wote
wakiwemo walimu lakini akawataka kufanya kazi kwelikweli kwa kuwa
hataweza kuwavumilia wazembe.
Pia Dr Magufuli ambaye amekuwa akitumia usafiri wa barabara kwa
kile anachokisema ni kujionea kero za watanzania badala ya kusimuliwa
hii leo pekee ametembea kilomita zaidi ya 435 za barabara ya vumbi huku
akiwaahidi watanzani kutowaangusha lakini pia akawasisitiza watanzania
kumchagua rais anayeaminika lakini pia atakayedumisha ujirani mwema na
nchi jirani pamoja na wahisani.
Jumatano ya September 02 Dr Magufuli anatarajiwa kuendelea na ziara
yake mkoani Mtwara katika maeneo ya Newala, Tandahimba, Kitama Nanyamba
Mtwara vijiji ni ziwani na baadae mtwara mjini kwenye uwanja wa
mashujaa.
Post a Comment