Bondia
na mwanamichezo tajiri zaidi duniani Floyd ‘money’ Mayweather amemtupia
maneno ya kejeli bondia mwenza Manny Pacquiao kwamba inabidi asubiri
yeye astaafu ndio atabaki kuwa bondia bora.
Floyd ameyasema hayo akiwa MGM
Arena kujiandaa na pambano lake la mwisho dhidi ya Andre Beto ambalo
litakua la 49 na kwamba hatopigana tena. Floyd akasema pamoja
kunamabondia wengi kwenye game ya ngumi, lakini uzoefu utambeba Pacquiao
kuwa bora pindi yeye akistaafu.
Kauli hiyo ya Mayweather ni ya
kejeli kwa Pacquiao ambaye alimchukia tangu alipotangaza kuwa alipigana
na Mayweather akiwa na maumivu ya bega kitu kilichomuudhi Floyd
aliyeamini Manny Pacquiao analeta visingizio badala ya kukubali matokeo.
Bondia Floyd Mayweather atapanda
ulingoni tarehe 12 mwezi huu kupambana na Mmarekani mwenza Andre Berto
katika pambano lake la mwisho la career yake ya ngumi na kama akishinda
basi atakua ameweka rekodi ya aina yake ya kutopoteza hata mchezo mmoja
kwani hadi sasa ameshinda michezo yote 48 aliyocheza.
Post a Comment