Mke wa rapa Kanye West, Kim Kardashia ametumia muwakilishi wake
kuzungumzia ripoti zilizosambaa kwenye mitandao zikidai kuwa ana mpango
wa kuchukua video wakati anajifungua mtoto wa pili.
Taarifa hizo za awali zilizoripotiwa na mtandao wa Hollywoodlife
zilieleza kuwa star huyo wa ‘Keeping Up with the Kardashians’ alikuwa na
mpango wa kushuti video hiyo licha ya ukweli kuwa alifanya hata sura ya
mwanae wa kwanza North West kuwa siri kubwa kwa kipindi kirefu.
Muwakilishi wa Kim Kardashian amekanusha taarifa hizo na kudai kuwa
hazina ukweli wowote. Muwakilishi huyo aliyezungumza kwa niaba ya Kim K
alikanusha pia tetesi za awali kuwa Kanye West alikuwa anataka mtoto wao
North West kuwa katika chumba cha kujifungulia wakati Kim atakapokuwa
akimleta duniani mdogo wake.
Post a Comment