Kiongozi wa G –Unit, 50 Cent ametuliza minong’ono ya waliokuwa wanasubiri aanze kuwauzia vitu baada ya kutangaza kufilisika.
Rapa huyo ameonesha bado anazo za kutosha baada ya kuonesha nyumba
yake mpya ya kifahari anayomalizia kuijenga iliyopo barani Afrika.
Mwezi Julai mwaka huu, 50 Cent aliamriwa na mahakama kumlipa fidia ya
dola milioni 5 mwanamke ambaye alimdhalilisha kwa kuvujisha mkanda wake
wa ngono.
Licha ya kuwa Forbes ilimtangaza kuwa na utajiri wa dola milioni 155,
rapa huyo aliiambia mahakama kuwa hana kitu na kwamba anakaribia
kufilisika. Aliitaka mahakama kutoamini mbwembwe anazopost kwenye
mitandao.
Post a Comment