Licha
ya serikali kufunga migodi 5 yenye migogoro ya mitobozano katika mgodi
wa Tanzanite wa Milerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, uongozi wa
chama cha ushirika wa wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite umepata
wakati mgumu wa kuzima jaribio la genge la wachimbaji wadogo zaidi ya
200 maarufu kama wanaapolo kutaka kuvamia mgodi wa madini wa Tanzanite
one unaomilikiwa na wawekezaji wa ndani wakipinga mwekezaji huyo
kuwateka baadhi ya wachimbaji wenzao ndani ya mgodi huo kwa lengo la
kupora madini.
Wakizungumzia tukio hilo lililotokea katika eneo la kitalu “B”
wachimbaji hao wamesema mwekezaji huyo alitumia mwanya huo kwa askari
wake kuvamia mgodi usiokuwa na mtobozano mali ya Bw Saidi Nasoro
Mwarabu mara baada ya kiberenge chake kuharibika na wakati walipokuwa
kwenye matengenezo waligundua moshi uliokuwa ukitoka ndani ya mgodi huo
na walipofuatilia ndipo walipokutana na moshi unaodhaniwa kuwa
umesababishwa na mabomu ya askari wa mwekezaji huyo wakati wakitekeleza
azma hiyo, na hali ilikuwa hivi.
Hata hivyo baada ya kukubaliana na ushauri wa mwenyekiti wa
ushirika huo, ndipo walipoeleza kushangazwa na hatua ya mwekezaji huyo
kutumia mwanya huo, hasa baada ya kuona mgodi huo ndio unaonyesha neema
ya kupatikana kwa madini ya Tanzanite wakilalamikia askari hao kukiuka
sheria, kanuni na utaratibu wa kuingia na silaha ndani ya mgodi.
Hata hivyo licha ya jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi
zikiendelea, meneja mahusiano wa kampuni hiyo ya Tanzanite One Bw
Khalfani Mbezi alipoulizwa juu ya vurugu hizo amesema wachimbaji hao
wamekuwa wakikiuka sheria kwa kuvuka mipaka na kuingia ndani ya eneo la
Tanzanite One.
Post a Comment