Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Montreal Impact inyoshiriki Ligi Kuu Marekani (MLS), ameanza vizuri katika mechi yake ya kwanza toka ajiunge na Ligi hiyo.
Drogba aliyejiunga na timu hiyo kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea, alifanikiwa kuifungia timu hiyo goli 3 (hat-trick) katika ushindi wa goli 4-3 dhidi ya klabu ya Chicago Fire. Huo ni mwanzo mzuri kwa staa huyo wa Afrika katika Ligi Kuu Marekani.
Post a Comment