Kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kilisafiri Jumamosi ya September 5 kuelekea Albania kucheza mechi ya kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Euro 2016. Mchezo utapigwa Jumatatu ya September 7, muda mchache kabla ya kuanza safari ya kuelekea Albania ambapo watafikia katika mji mkuu wa nchi hiyo Tirana.
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo pamoja na winga wa klabu ya Besiktas, Ricardo Quaresma waliingia
katika chumba cha rubani na kupiga picha na video, ambayo muda mchache
baadae ilianza kuenea katika mitandao ya kijamii, hii ilikuwa kabla ya
ndege kuanza safari ya kuelekea Albania.
Post a Comment