Klabu ya Manchester United ya Uingereza ipo karibuni kumsajili mshambuliaji chipukizi kutokea Monaco ya Ufaransa, licha ya kuwa bado haijathibitika kuwa wamemsajili ila tayari Anthony Martial ameripotiwa kufanya vipimo vya afya katika klabu ya Manchester United.
Anthony Martial anaripotiwa kusajiliwa na Man United
kwa dau la pound milioni 36, kulingana na umri wake kuwa mdogo, kiasi
hicho kinatajwa kuwa sio cha kawaida kiasi kwamba kimepelekea nahodha wa
timu hiyo Wayne Rooney kushituka kidogo na kumuuliza Morgan Schneiderlin kuhusiana na mshambuliaji huyo.
“Kiukweli
wakati tupo katika ndege Wayne Rooney alikuja kuniuliza Martial ni nani?
kwa sababu magazeti ya Uingereza yalikuwa yakimzungumzia, nilimwambia
ni mchezaji mzuri ana uwezo mkubwa na alicheza mechi kadhaa na Monaco
msimu uliyopita na mwanzoni mwa msimu huu”>>>Morgan Schneiderlin
“Nilimwambia
Rooney kiufundi yupo vizuri na anafananishwa na Thierry Henry hata
hivyo ni kwa mujibu wa magazeti ndio yanayomfananisha na
Henry”>>> Morgan Schneiderlin
Anthony Martial
ni mchezaji mwenye umri wa miaka 19 hivyo wengi ulinganisha kiasi cha
fedha na umri wake, kwani mara nyingi mchezaji anaye nunuliwa kwa dau
kama hilo ni mchezaji mkubwa au kama mdogo ni lazima awe na uwezo
mkubwa, hivyo ndio maana Rooney amebidi aulize kuhusiana na mchezaji huyo.
Post a Comment