Mrembo Jokate Mwegelo amepata shavu la kuwa mtangazaji ‘Talk Show’ mpya itayorushwa kwenye channel za Star Times.
Jokate ambaye amefanya kazi za utangazaji na vituo vikubwa vya
runinga Afrika, anatarajiwa kuwa nyota ya kuing’arisha ‘Talk Show’ hiyo
iliyopewa jina la Mashariki Max itakayolenga katika kuonesha utamaduni
wa maisha ya Afrika Mashariki.
“Nimekuwa nikihost shows nyingi, lakini naamini Mashariki Max itanipa
uzoefu zaidi na itanisaidia katika career yangu kwa sababu watu wengi
wataniona kwa sababu show itarushwa na Star Times kupitia ST Swahili
Channel,” Jokate aliwaambia waandishi wa habari.
Kipindi hicho kitakachotumia lugha ya Kiswahili, kitaanza kurushwa hivi karibuni kuanzia majira ya saa kumi na mbili na nusu.
Jokate ni mtangazaji wa vipindi vya runinga mwenye vipaji vingi ikiwa ni pamoja na uigizaji, uimbaji na urimbwende.
Post a Comment