Baada ya miaka miwili ya ukimya katika muziki, mkali wa ‘Muhogo
Andazi’, Nuru The Light amerejea na wimbo mpya alioupa jina la ‘L’.
Nuru ambaye muda mwingi alikuwa nchini Sweden, wiki iliyopita
aliachia huo ambao umetayarishwa kwa kiwango kizuri cha muziki wa ‘Live’
katika studio za Joevibes Production, zilizoko nchini Sweden.
Akiongea na Dar 24, Nuru amesema kuwa ‘L’ katika wimbo huo wa mapenzi
ina maana nyingi kubwa na chanya ambazo heruhi hiyo inaziwakilisha.
“‘L’ ina simamia vitu vingi positive, inaweza kuwa Love, Lough, Life
na nyingine,” alisema. “Jina la wimbo huu linatokana na ubunifu na
kuonesha kuwa hata herufi moja tu inaweza kusimamia wimbo mkubwa kama
huu na ukafanya vizuri,” aliongeza.
Nuru ambaye aliwahi kufanya vizuri na nyimbo kama Muhogo Andazi,
Walimwengu, Msela na Nsubiri Usilale amekamilisha video ya ‘L’
aliyofanya na muongozaji mkongwe, Adam Juma na hivi karibuni atarajia
kuizindua kwa njia ya kipekee.
“Nashukuru Adam Juma hajawahi kuniangusha katika video zote, hii
video ya ‘L’ ni nzuri sana na naamini mashabiki wangu wataipenda kwa
moyo wote. Nakamilisha mipango ya uzinduzi wa video, utakuwa wa kipekee,
baada ya hapo mtaiona kwenye TV na mitandaoni,” alisema.
Mwimbaji huyo wa kike ambaye ameishi Sweden kwa muda mrefu na hivi
sasa yuko nchini kwa ajili ya kusimamia projects zake kadhaa, amewaahidi
mashabiki wake kuwa ingawa yuko ughaibuni, hatawaangusha na ataendelea
kufanya muziki mzuri kwa ajili ya nyumbani Tanzania.
Post a Comment