Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu
Lissu, amesema tuhuma zilizotolewa na aliyekuwa katibu mkuu wa chama
hicho Dr Wilibrod Slaa, si za kweli na anaongozwa na tamaa za madaraka.
Akizungumza jana jioni na redio idhaa ya kiswahili ya DW, Tundu
amedai Dr Slaa ndio alihusika kufanya mpango wa kumkaribisha mgombea
Urais wa UKAWA Edward Lowassa CHADEMA na si vinginevyo.
“Mshenga ni Gwajima hajajisema yeye mposaji, kilichoharibika ni First
Lady mama alikataa siku ambayo kamati kuu ilimpokea Lowassa Dr alilala
nje alitupiwa mabegi yake akalala kwenye gari kesho yake akasema hataki
anataka kujiuzulu.
kama nmemsikia sawa sawa amesema yeye hana chama, juzi amepokea
mshahara wa chama, nyumba anayokaa imenunuliwa na chama walinzi alionao
ni wa chama, anatukana chama wakati bado amechukua mshahara wa ukatibu
mkuu wa chama juzi”
Katika ‘line’ nyingine, Lissu ameongeza kuwa Lowassa alihojiwa na
kamati kuu kuhusu kashfa za ufisadi wa Richmond, na kudai aliyefanikisha
mkataba kusainiwa ni Rais Kikwete si yeye (Lowassa).
Post a Comment