Hatimaye aliyekuwa mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ameibuka na
kuzijibu hoja za Dk. Wilbroad Slaa kuwa yeye ni fisadi aliyeshirikiana
na Edward Lowassa katika sakata la Richmond na kwamba alimtishia kumuua.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Rostam amedai kuwa Dk Slaa
ni muongo mkubwa na kumtaka Dk Slaa kujitokeza tena na kutoa ushahidi
wa kutosha kuwa alimtishia maisha.
“Nilishitushwa na nilisikitika sana, ingawa sikushangaa kusikia
tuhuma za Dk Slaa dhidi yangu. Sijawahi kuwa na mawasiliano ya moja kwa
moja naye na madai kuwa nilimtishia maisha yanapaswa kupuuzwa kwa sababu
hayana msingi. Kwa nini hakuniripoti polisi badala ya kusubiri miaka
yote hiyo kuja kuzungumza hadharani?” Alihoji Rostam Aziz.
Rostam asema kuwa amekuwa na mazoea ya kutoa maneno ya uongo dhidi ya
yake na kwamba mwaka 2010 aliwahi kusema kuwa yeye, Edward Lowassa na
rais Jakaya Kikwete walikuwa na mkutano Mwanza katika hotel ya Lakairo
wakipanga jinsi ya kuhujumu uchaguzi mkuu. Lakini wakati anatoa taarifa
hizo, Rostmam anadai yeye alikuwa Afrika Kusini, rais Kikwete alikuwa
Lindi na Lowassa alikuwa Arusha.
Katika hatua nyingine, Rostam alikanusha kuhusika na kuifadhili Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Rostam Aziz alitangaza kujiuzulu siasa mwaka 2011 akiliacha wazi
jimbo la Igunda na kueleza kuwa amechoshwa na siasa za kuchafuana.
Post a Comment