Watanzania
wametakiwa kujenga tabia ya kudadisi,kuchunguza na kuwapima wagombea
kwa sera zao ili kuepuka kuchagua viongozi wabovu kwakuwa watanzania
wanahitaji viongozi watakaoleta mabadiliko ya kidemokrasia na kuikwamua
Tanzania katika wimbi la umasikini hali inaosababishwa na viongozi
wachache wanaotumia nafasi zao kujinufaisha wenyewe.
Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni za uchaguzi jimbo la Kahama
mjini mbunge anayetetea nafasi yake kwa tiketi ya Chadema Mh.James
Lembeli amesema wagombea wanaoomba kura kwakuwahonga wananchi hafafai
huku akiwataka wananchi wa kahama kuchagua viongozi watakaoweza kufanya
kazi ya kuleta maendeleo na sio kwenda bungeni kufanya mahesabu ya
biashara zao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kanda ya Serengeti Chadema
Bw.Sylivesta Kasulumbai amesema hoja ya wasukuma sio kumuona Msukuma
anaingia ikulu bali ni kumpata kiongozi muadilifu bila kujali kabila
wala dini yake huku mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la
kishapu Bw.Fred Mpendazoe akiwataka watanzania kudadisi,kuchunguza na
kujiuliza kwanini viongozi wakubwa wa chama cha mapinduzi wanatoka na
kuhamia vyama vingine.
Post a Comment