Siku
moja baada ya mamlaka ya hali ya hewa nchini kutoa tahadhali ya mvua
kubwa katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera imenyesha mvua kubwa ya mawe
iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha maafa makubwa ambapo kaya
312 zimeathirika vibaya kwa kukosa chakula baada ya mashamba yao
kusombwa na maji huku familia sita zikikosa makazi na baadhi ya majengo
ya shule ya msingi na jengo moja la halmashauri ya wilaya kuezuliwa na
upepo.
Mvua hivyo iliyoanza kunyesha majira ya saa kumi na mbili jioni
imesababisha madhara makubwa kwa wananchi wa mji wa Ngara ambapo
mashamba ya migomba ya ndizi yamehalibiwa vibaya huku nyumba zikiezuliwa
na upepo ambapo ITV imezungumza na afisa mtendaji wa kata ya Ngara
mjini Bw.Yothamu John amesema kuwa mvua hivyo imesababisha madhara
makubwa kwa jamii.
Baadhi ya waathirika wa mvua hivyo wameiomba serikali kuwasaidia
misaada mbalimbali ikiwemo chakula ili kunusuru maisha ya watu
wanaokabiliwa na janga la njaa kutokana na mazao waliyokuwa wakitegemea
kwa chakula kusombwa na maji.
source: ITV
Post a Comment