Wachezaji watatu wa kimataifa wa Tanzania wanacheza soka la
kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa (Free State – Afrika Kusini) Thomas
Ulimwengu na Mbwana Samatta (TP Mazembe – Congo DRC) wamejiunga na kambi
ya Taifa Stars iliyopo katika hoteli ya Urban Rose – Kisutu jana jijini
Dar es salaam.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charels Mkwasa amewapokea wachezaji hao na
jana kufanya mazoezi pamoja na wachezaji waliokuwa kambini nchini
Uturuki saa 10 jioni katika uwanja Taifa jijini Dar salaam.
Kwa mujibu wa ratiba ya kocha Mkwasa Stars leo alhamis itaendelea na
mazoezi jioni saa 10 katika uwanja wa Taifa kabla ya kufanya mazoezi
mepesi ya mwisho kesho ijumaa asubuhi.
Wachezaji waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa, Said Mohamed,
walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein,
Kelvin Yondani, Hassan Isihaka na nahodha Nadri Haroub “Cannavaro”.
Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Said Ndemla, Salum
Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva na Farid Musa, huku safu ya
ushambuliaji ikiwa na John Bocco, Rashid Mandawa, Ibrahim Ajib, Thomas
Ulimwengu, Mrisho Ngasa na Mbwana Samatta.
Post a Comment