Baada ya harakati za kutaka kuihama Man Utd na kujiunga na klabu
ya Real Madrid katika usajili wa majira ya kiangazi kukwama, mlinda
mlango kutoka nchini Hispania David de Gea Quintana, amejumuishwa kwenye
kikosi cha wachezaji 23 kitakachopambana kwenye michuano ya ligi ya
mabingwa barani Ulaya msimu wa 2015-16.
De Gea alikua aliachwa pembeni ya kikosi cha Man utd ambacho kilikua
na mtihani wa kufuzu kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo, dhidi ya
Club Brugge ya nchini Ubelgiji, kwa kusudio la kuangalia uwezekano kama
angeweza kutimiza ndoto zake za kurejea nyumbani Hispania.
Kujumuishwa kwenye kikosi hicho, kunaamisha mambo yamekaa sawa sawa
kwa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 24, na sasa huenda akawa
sehemu ya wachezaji ambao watarejeshwa kwenye kikosi cha kwanza kufuatia
uwezo mkubwa alionao.
Hata hivyo katika orodha hiyo iliyowasilishwa UEFA, jina la aliyekua
mlinda mlango wa FC Barcelona, VÃctor Valdés Arribas limeachwa, hivyo
hatoweza kucheza michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya klabu.
Valdes amekua na mkwaruzano na meneja wa klabu ya Man Utd, Louis Van
Gaal tangu mwezi July wakati kikosi cha mashetani wekundu kilipokua
kikijiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi unaoendelea.
Kwa sasa De Gea amerejea nyumbani Hispania kuitikia wito wa timu ya
taifa lake, ambayo itakua na mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali
za mataifa ya barani Ulaya dhidi ya Slovakia pamoja na Macedonia.
Katika orodha ya Man utd iliyowasilishwa UEFA, tayari kwa kupambana
kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, wapo
wachezaji wote waliosajili katika kipindi cha majira ya kiangazi kama
Anthony Martial aliyesajiliwa siku ya mwisho ya dirisha la usajili
akitokea AS Monaco kwa ada ya paund million 36, mlinda mlango Sergio
Romero, Matteo Darmian, Bastian Schweinsteiger, Morgan Schneiderlin
pamoja na Memphis Depay.
Kikosi cha Man Utd kitakachopambana na kuhakikisha kinajitetea kwenye
mipango ya kutwaa ubingwa wa barani Ulaya msimu wa 2015-16, upande wa
makipa yupo David De Gea, Sergio Romero, Sam Johnstone
Mabeki: Phil Jones, Marcos Rojo, Chris Smalling, Luke Shaw, Guillermo Varela, na Paddy McNair.
Viungo: Michael Carrick, Daley Blind, Ashley
Young, Ander Herrera, Nick Powell, Antonio Valencia, Marouane Fellaini,
Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger, Jesse Lingard, Andreas
Pereira na Juan Mata
Washambuliaji: Memphis Depay, Anthony Martial, Wayne Rooney na James Wilson
Post a Comment