Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi ambaye ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa,
James Mbatia amezungumza kwa niaba ya Ukawa, kuhusu tuhuma zilizotolewa
jana na Dk. Wilbroad Slaa dhidi ya Edward Lowassa na Chadema.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mbatia
amesema kuwa Dk. Slaa aliudanganya umma kwa kukataa kuwa hakutangaza nia
ya kugombea urais kupitia Ukawa kwa kuwa walikaa pamoja na yeye akasema
ni bora zaidi.
“Wagombea wetu wa urais walikaa pamoja, na Dk. Slaa alisema wazi kuwa
yeye ni bora zaidi ya wote, sasa leo anasema hakuwahi kutia
nia,kweli?,” alihoji.
Alidai kuwa Dk. Slaa aliudanganya umma kwa kusema yeye ni msafi huku
akidai kuwa alikataa rushwa ya shilingi milioni 500 mwaka 2007 na
hakuwahi kusema suala hilo hadi jana alipokuwa akimzungumzia Edward
Lowassa.
“Eti suala la rushwa zaidi ya miaka 7 usiripoti halafu uje useme leo, kusema uongo ni kazi sana,” alisema Mbatia.
Aidha, alimkosoa Dk. Slaa kwa kuwahusisha maaskofu na vita ya kisiasa
inayoendelea huku akiwaomba radhi watumishi hao wa dini kwa kile
kilichosemwa dhidi yao akidai kuwa ni vyema angeacha wanasiasa wasuguane
wenyewe bila kuwasisha viongozi wa dini.
Mbatia meeleza kuwa tukio hilo ni mfululizo wa matukio yanayofanywa
na CCM katika kutafuta namna ya kuiyumbisha Ukawa na kuitoa kwenye reli
ili iache hoja za msingi za kampeni na kuanza kumjibu mtu mmoja mmoja.
“Hivi ni ashiria kwamba CCM wameshindwa hoja, mara kuleta mambo ya
udini, mara wanaibua hili mara lile. wanataka kuchafua amani yetu kwa
kuigiza masuala ya dini.”
Katika hatua nyingine, mbatia amewataka wajumbe wa kamati ya siasa ya
CCM, Samuel Sitta na Harison Mwakyembe wanaotafuta kufanya mdahalo na
Lowassa kumuacha apumzike kwa kuwa mgombea huyo wa urais sio saizi yao
na kwamba kama wanataka mdahalo wamualike yeye.
Mbatia pia alihoji sababu za Dk. Slaa kumvaa Frederick Sumaye wakati
hoja yake ilikuwa ni Edward Lowassa na sio mtu mwingine kama alivyodai.
“Tukisema tuibue masuala yote na kashifa za kuuzwa kwa nyumba, kuna mtu atabaki salama?” Alihoji.
Aliwataka watanzania kuendelea kushikamana kuhakikisha wanakamilisha
nia yao ya kuipata katiba mpya ambayo hivi sasa inaongozwa na Edward
Lowassa.
Post a Comment