Timu ya taifa ya Tanzania na Nigeria September 5 zimekutana kucheza mechi ya kuwania tiketi ya kufuzu kucheza AFCON 2017, ikiwa ni zaidi ya miaka 20 toka zikutane katika mechi za mashindano. Nigeria inayonolewa na kocha mzawa Sunday Oliseh ndio imecheza mechi ya kwanza toka ianze kufundishwa na kocha huyo.
Kwa upande wa Taifa Stars ambayo haina point hata moja katika kundi lake baada ya kufungwa mchezo wa kwanza na timu ya taifa ya Misri kwa jumla ya goli 3-0, imeshuka uwanjani kuwania point 3 ili iweze kukufua matumaini ya kupata tiketi ya kucheza AFCON 2017.
Mechi iliyochezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam imemalizika kwa timu zote kutoka sare ya bila kufunga, japo Taifa Stars kupitia kwa Mrisho Ngassa na Thomas Ulimwengu ilipoteza nafasi mbili za wazi.
Hizi ni picha za mechi hiyo mtu wangu.
Post a Comment