Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli ameendelea
kutangaza vita dhidi ya ufisadi akijifananisha na maji ya moto dhidi ya
mafisadi.
Akiongea na waanchi mkoani Mtwara, Magufuli aliwafananisha mafisadi
na ‘kunguni’ waliojificha kwenye kitanda ambao dawa yao ni kuwamwagia
maji ya moto.
“Mimi ni maji ya moto wa mafisadi, nipeni urais muone nitakavyowaunguza,”alisema Dk. Magufuli.
Katika hatua nyingine, Dk. Magufuli alisisitiza kuwa atahakikisha
anamaliza tatizo la maji katika mkoa huo na kwamba waziri wa maji
atakayemchagua hatakaa Dar es Salaam na kusherehekea wiki ya maji wakati
wananchi hawana maji.
Post a Comment