Akitangaza uamuzi huo wa tume mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Salum
Kassim Ali amesema tume imeridhika na wagombea hao wakiwemo CCM, CUF na
TADEA na sasa na majina hayo yatabandikwa nje kwa masaa 24 ili kama
kutakuwa na pingamizi watapitia na kutolea maamuzi ndani ya masaa 24.
Mapema wagombea wa vyama 10 kati ya 11 waliobaki walikamilisha
utaratibu wa tume ya kuwasilisha fomu na ada ya shilingi milioni mbili
huku mgombea wa mwisho wa chama cha NRA Seif Ali Iddi aliwasilisha fomu
zake kukiwa kumesalia dakika 3 bada ya kupata ajali akiwa njiani kuja
ofisi za tume, hata hivyo alifanikiwa na tume kumpokea na jina lake
kubandikiwa kuwa mgombea urais wa Zanzibar.
Wagombea wengine waliofika wakati wa asubui katika ofisi za tume ni
pamoja na mgombea wa chama cha Jahazi asilia Kassim Bakari Ali ambaye
alifika akiwa katika gari maalum na baadaye akafuata mgombea wa ADC Bw
Hamad Rashid akiwa ameonganzana na wafuasi wa chama hicho ambapo
wagombea wote hao walilia haki na huru katika uchaguzi mkuu.
Kampeni za urais wa Zanzibar zinatarajiwa kuanza rasmi kuanzia
jumatatu jioni huku kukiwa hakuna dalili ya kuwepo pingamizi kutoka kwa
mgombea yeyote, zoei hilo limeshudia wagombea 15 wakijitokeza kuwania
urais wa Zanzibar mwaka huu tafauti na uchagzui ulipita walikuwa
wagombea saba, chama pekee amabcho
kimeshindwa kurejesha foumu ni cha updp ambaye mgombea wake alikuwa mwanmke mwajuma ali khamis.
Post a Comment