Klabu ya AC Milan, imethibitisha itamkosa kiungo Andrea
Bertolacci katika mchezo wa ligi ya nchini Italia wa mwishoni mwa juma
hili baada ya kuumia paja akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa.
AC Milan wamelazimika kutoa taarifa hizo kufuatia joto la mchezo
utakaowakabili dhidi ya Inter Milan kuendelea kupanda miongoni mwa
mashabiki wa soka wa mjini Milan, kwa kuamini mambo yatakua magumu kwa
kila upande.
Bertolacci, aliondolewa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Italia na
kurejeshwa klabuni kwake, baada ya kufanyiwa vipimo na kubainika
anakabiliwa na majeraha ya paja ambayo yatamuweka nje kwa siku kadhaa
zijazo.
Taarifa hizo za kukosekana kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24,
zimepokelewa kwa huzuni na mashabiki wa klabu ya AC Milan ambao
wameonyesha kumkubali tangu mwanzoni mwa msimu huu baada ya kusajiliwa
akitokea Genoa kwa ada ya Euro million 20.
Post a Comment