Mgombea wa Urais wa Ukawa Edward Lowassa  pamoja na mgombea mwenza Juma Duni Haji leo wamewashitukiza wafanyabiashara  katika soko la Tandika jijini Dar es salaam.

Aidha, wagombea hao waliwasili katika soko hilo asubuhi ya leo ambapo shughuli zilisimama kwa muda.


Kabla ya kuanza mazungumzo na wafanyabishara  hao,Lowassa   alikaribishwa  chai  na mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo.

Ziara hiyo ya kushitukiza iliyoanzia Mbagala siku ya jana ni maalumu kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa hali ya chini kuhusiana na matatizo yanayowakumba  katika maisha yao ya kila siku.

Je, Unataka kufahamu kesho Lowassa atakuwa wapi? Endelea kufuatilia mtandao  huu.


Post a Comment