Unywaji kidogo wa pombe hadi chupa
moja kwa siku kwa wanawake na chupa mbili kwa wanaume unaweza
kusababisha hatari ya kupata saratani kulingana na watafiti.
Makala moja ya Uingereza ilichambua utafiti mkubwa kutoka nchini Marekani uliofanyiwa zaidi ya watu 100,000.
Wataalamu wanasema kuwa matokeo hayo yanatuma ujumbe wa kiafya kuwa watu wanahitaji kupunguza kiwango cha pombe wanachokunywa na mara nyinge hata kuwa na siku ambazo hawanywi pombe.
Mara nyingi inahitajika kuwa wanaume wanaweza kunywa zaidi ya chupa tatu kwa siku na wanawake zaidi ya chupa mbili au tatu lakini huenda viwango hivyo vikafanyiwa marekebisho.
Watafiti hao pia waligundua kuwa hatari inayotoka na unywaji wa pombe hasa satarani ya matiti iliongezeka hata kwa kunywa chupa moja ya pombe kwa siku.
Post a Comment