Bw.Makene ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la
vyama vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao
wametumia nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na
watendaji wa serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama
tawala.
Viongozi hao wa vijana wamesema hatua ya viongozi na watendaji wa
serikali ya kujihusisha moja kwa moja na kampeni za CCM huku wengine
wakitumia rasilimali za umma na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya
upinzani inathibitisha ukweli wa malalamiko yao.
Post a Comment