Muda mfupi kabla mgombea ubunge kwa
tiketi ya CHADEMA jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Bw.Fred Mpendazoe
kurudisha fomu baadhi ya wanachama wa chama hicho wameandamana na
kuvamia ofisi ya chama kwa madai kuwa hawakubaliani na kitendo cha
kamati kuu ya wilaya kubadilisha matokeo ya kura za maoni na kumtangaza
mgombea wasiyemtaka kugombea nafasi hiyo.
Wakizungumza na ITV baadhi ya wanachama hao wamedai kutokubaliana
na mapendekezo ya kamati kuu kubadilisha jina la mgombea wao Bw.Donald
Kahema waliyekuwa wamemchagua kwa kura mia mbili tisini dhidi ya Fred
Mpendazoe aliyepata kura kumi na moja hali inayoonyesha baadhi ya
viongozi wanakitumia chama vibaya kwa maslahi binafsi na kutishia
kuvuruga chama ambacho wananchi walikiamini kwa muda mrefu kuwa kinaweza
kuleta mabadiliko ya kidemokrasia.
Aidha katibu muenezi chadema wilaya ya kishapu Bw.Martin Ganja
amekiri kuwepo kwa hali hiyo huku akidai kuwa kamati kuu imekiuka na
kupora haki za msingi za wapiga kura na yeye kama kiongozi atasimama
imara na kuhakikisha kuwa anapigania haki na maslahi ya wanachama.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chadema wilaya ya kishapu Bw.Paulo
Magembe amesema kimsingi wanachama wana haki ya kudai haki zao huku
akidai kuwa kamati kuu ina wajibu wa kuona ninini wanachama wake
wanahitaji ili kukiepusha chama kuingia katika migogoro inaoweza
kusababisha chama kuanguka katika uchaguzi mkuu ujao.
source by ITV
Post a Comment