Mhlowasa aliyeambatana na mgombea mwenza Mh.Duni Haji baada ya
kufika katika kituo hicho hakuishia tu kuwatazama wananchi
wanavyotaabika na usafiri bali aliungana nao kusafiri kwa kutumia moja
ya dala dala inayotoka Gongo la Mboto kwenda Kisarawe na kushuka
chamazi na kisha akatumia usafiri wa gari ndogo za abiria aina ya Noah
kutoka chamazi hadi Mbagala.
Licha ya kuwa ziara hiyo ilikuwa ni ya kustukiza ilivuta umati
mkubwa wa watu wa rika mbali mbali wengi wakiwa vijana ambao waliacha
shughuli zao na kuanza kuwafuata viongozi hao wakitaka kusikia walau
sauti zao na licha ya mgombea mwenza Mh.Duni Haji kuwatuliza kwa
kuwaeleza kuwa watazungumza nao baada ya uzinduzi wa kampeni
waliendelea kuwafuata viongozi hao.
Wananchi waliokuwa kwenye maeneo hayo wamesema hatua ya viongozi
hao wa ukawa ya kufika kujionea wao wenyewe taabu na shida
zinazowakabili licha ya kuwapa matumaini ya kuondokana na tatizo hilo
inadhihirisha adhima ya umoja wa ukawa ya kuleta mabadiliko
yaliyoshindikana kwa zaidi ya miaka hamsini.
Post a Comment