MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Mbunge wa Urambo aliyemaliza muda wake, Samuel Sitta ametaka uandaliwe mdahalo kwenye vyombo vya habari kati yake na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa uelezwe ukweli juu ya ukweli wa sakata la Richmond.
Sitta
ambaye alikuwa Spika wa Bunge wakati Lowassa alipojiuzulu kutokana na
sakata hilo, alisema katika mdahalo huo, ataeleza ukweli juu ya uhusika
wa Lowassa katika sakata hilo na atatoa vielelezo kueleza taifa ufisadi
uliokuwa ukifanyika.
Alisema
hayo jana kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM mkoa wa Shinyanga katika
mkutano uliofanyika mjini hapa ambao wagombea wa udiwani na ubunge wa
majimbo yote ya mkoani hapa walitambulishwa.
Katika
mkutano huo, alisema kujiuzulu kwa Lowassa mwaka 2008, kulitokana na
Kamati Teule iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe, kugundua kwamba
fedha za walipa kodi zilikuwa zikipotea bure.
Alisema yuko tayari kusimulia kwa umma utajiri wa mgombea huyo wa Chadema.
Makundi, urafiki
Sitta ambaye ni Waziri wa Afrika Mashariki, ambaye pia alikuwa kwenye kinyang’anyiro cha kutaka kuteuliwa kugombea urais kupitia CCM, alisema wanamwamini Dk John Magufuli katika utendaji wake wa kazi na pia ni kiongozi asiye na makundi au urafiki.

“Kweli
lazima uwapime viongozi, kwani anayetaka urais lazima achaguliwe kwa
kufuata utaratibu, achambuliwe usiogope moshi kama unapikia kuni…lakini
mwenzetu Lowassa hakukubaliana na hayo, akaona kaonewa kwa madai anafaa
kuwa rais mbona sisi tulikubali?,” alihoji Sitta.
Aliendelea kusema, “hali
hiyo, ilionesha ndani ya CCM kulikuwa na vyama viwili ambavyo ni ‘CCM
Katiba’ na ‘CCM Maslahi’ ambayo alikuwa anaongoza Lowassa na mfuasi
wake, Mgeja (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia
alihamia Chadema hivi karibuni).”
Wanachama mapandikizi
Sitta alisema CCM ilikuwa imejaa wanachama walio mapandikizi tofauti na sasa ambapo alidai wamekwisha jionesha na kimekuwa chama kizuri kama ilivyokuwa enzi za hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Alisisitiza kwamba kitazidi kuimarika na waliobaki wataendelea kutetea ilani na kuhakikisha chama kinaendelea kushika dola.
Kwa mujibu wa Sitta, wakati wa mchakato, baada ya kumaliza vikao, Lowassa alikuwa akiitisha vikao vya kundi lake alilolibatiza CCM Maslahi na kuwaagiza wapambe wake kuitisha vyombo vya habari kushambulia watu ambao hawako kwenye mlengo wao.

Wakati
huo huo mjumbe huyo wa NEC, alikumbusha umati uliohudhuria mkutano huo
kwamba, uchaguzi wa mwaka huu unatumia Katiba ya zamani ya mwaka 1977
ambayo inatamka matokeo ya rais hayahojiwi hata kama aliyeshinda,
amezidi kura moja.
Sitta
ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, alisema alishauri wabunge
wasitoke nje ya Bunge hilo waweze kutumia katiba hiyo iliyokuwa na
kipengele cha kuhoji matokeo ya rais sasa imekula kwao.
Post a Comment