Mwezi October 2014 iliytolewa hukumu ya
kifungo cha miaka mitano jela kwa kesi ya mauaji ambayo ilikuwa
inamkabili Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorious.
Stori nyingine iliyopewa uzito sasahivi
inahusu ishu ya Mwanariadha huyo kuachiwa kutoka gerezani Ijumaa ya wiki
hii August 21 2015 na kutumikia Kifungo cha nje, huku akiwa na jukumu
la kuripoti Kituo cha Polisi kila siku.
Oscar Pistorious alikuwa na kesi ya mauaji kutokana na tukio la kumpiga risasi aliyekuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp ndani ya nyumba yake.
Ripoti ya kuachiwa kwa Pistorious inakuja baada ya jamaa huyo kuwa tayari ametumikia miezi 10 jela tangu ahukumiwe na Mahakama Kuu ya South Africa.
Pistorious atakuwa
kwenye kifungo kwenye Jumba la Kifahari la mjomba wake huku akiwa na
kifaa maalum mguuni ambacho hatotakiwa kukivua hata mara moja, na
mwenendo wake utakuwa ukifuatiliwa wakati wote na watu wa usalama
kupitia kifaa hicho.
Uhuru mwingine ambao atakuwa nao ni wa kwenda mahali popote kwa ajili ya shughuli muhimu pamoja na kukutana na ndugu zake.
Japo inaonekana kifungo chake
kinaendelea kupata nafuu zaidi bado Wanasheria wanashughulika na
kuhakikisha Rufaa ya Kesi yake inasikilizwa ili kumlegezea adhabu ya
kifungo cha miaka mitano jela.
Stori nyingine toka jela zinaonesha jamaa anaishi maisha tofauti na wafungwa wengine >>> “Pistorious alikuwa ni VIP gerezani”—haya ni maneno ya mfungwa mmoja, Boswell Mhlongo ambaye walikuwa gereza moja la Kgosi Mapuru II, Pretoria.
Post a Comment