Mchezaji wa Manchester United Wayne
Rooney amesema ''magoli yatakuja'' baada ya kuanza msimu mpya bila ya
kufunga goli lolote.Rooney, mwenye miaka 29, amecheza kama mshambuliaji
wa kati kwenye michezo yote ya ufunguzi wa ligi.
Lakini bado hajafumania nyavu katika mchezo wowote tokea kuanza kwa msimu huku baadhi ya watu wakidai kuwa uwezo wake wa kufumania nyavu umeshuka.
''Nimekua na mchezo mbaya msimu huu na kilamtu analizungumzia hilo.Nimewahi kuwa na tatizo kama hilo kipindi cha nyuma lakini natumai mwishoni mwa juma nitafunga''alisema nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uingereza.
''Ndio kwanza msimu umeanza na tumecheza michezo mitatu peke yake.Nilitarajia haya na natumaini mabao yatakuja,najua hilo''Meneja wa Man United Louis van Gaal alimuacha washambuliaji Robin van Persie na Radamel Falcao huku akisalia na Rooney, Javier Hernandez pamoja na James Wilson kama safu yake kuu ya ushambuliaji.
Post a Comment